NSSF yawajengea uwezo wastaafu watarajiwa mkoani Mbeya
21 May 2024, 16:12
Katika kuhakikisha wafanyakazi kwenye taasisi zao wanapata haki zao,waajiri kulipa michango ya wafanyakazi wao kwa wakati ili kuwaondolea usumbufu pindi wanapostaafu.
Na Ezekiel Kamanga
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Kayuni amefungua mkutano wa Wastaafu Watarajiwa uliondaliwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) Jijini Mbeya.
Katika hotuba yake Kayuni amelitaka Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF kuanza kutoa elimu mara tu mfanyakazi anapoajiriwa.
Awali Meneja wa huduma kwa Wateja NSSF Robert Kadege amesema lengo ni kuwajengea uwezo Wastaafu Watarajiwa ili waweze kuelewa mambo mbalimbali ikiwemo kikokotoo.
Naye Meneja wa NSSF Mkoa wa Mbeya Deus Jandwa amesema wafanyakazi wawe na tabia za kufuatilia michango yao ya kila mwezi katika ofisi za NSSF.