Baraka FM

Wakristo washauriwa kuhudhuria mikutano ya injili

20 May 2024, 15:32

Mchungaji mwangalizi wa kanisa la Pentekost Holiness Mission (PHM) Mbeya jiji Magharibi John Ngonile

Wakristo wote ni vema kushiriki katika ibada za Pentekosti ili kukumbuka siku ya kuzaliwa kwa kanisa pamoja na ujazo wa Roho Mtakatifu.

Na Rukia Chasanika

Wakriso nchini wameshauriwa kuhudhuria katika mikutano ya pentekoste ili kujifunza neno la Mungu na kujazwa Roho mtakatifu kwa upya ikiwa ni ishara ya utakatifu mbele za Mungu.

Ushauri huo umetolewa na mchungaji mwangalizi wa kanisa la Pentekost Holiness Mission (PHM) Mbeya jiji Magharibi John Ngonile katika mkutano uliofanyika kanisa la PHM Kalobe mkoani Mbeya.

Sauti ya mchungaji mwangalizi wa kanisa la Pentekost Holiness Mission (PHM) Mbeya jiji Magharibi John Ngonile

Kwa upande wake katibu wa kanisa la Pentekost Holiness Mission Mbeya jiji Magharibi Daniel Kayange amesema maadhimisho ya siku ya pentekost yanasaidia wakristo kuinuka kwa upya katika kumtumikia Mungu.

Katibu wa kanisa la Pentekost Holiness Mission Mbeya jiji Magharibi Mchungaji Daniel Kayange
Sauti ya katibu wa kanisa la Pentekost Holiness Mission Mbeya jiji Magharibi mchungaji Daniel Kayange

Muhubiri katika mkutano huo Jacobo Mwakamisa amesema watumishi wa Mungu wanatakiwa kuhubiri kweli ya Mungu ili kuwasaidia watu kwenda mbinguni na sio kutaka sadaka pekee.

Baadhi ya wakristo walioshiriki katika mkutano huo Juma Maston Kalambile na Magreth Mwanyaje wamesema wamejifunza vitu vingi ikiwemo kuwa na msimamo na suala la Imani pamoja ujazo wa Roho mtakatifu.

Baadhi ya wake za wachungaji wa kanisa la PHM (Kushoto waliokaa)ni Rukia Chasanika mwandishi na mtangazaji wa Baraka fm
Sauti za baadhi ya wakristo walioshiriki katika mkutano huo Juma Maston Kalambile na Magreth Mwanyaje