Baraka FM

Viongozi wa machinga jiji la Mbeya waanza ziara katika masoko

20 May 2024, 10:51

Baadhi ya wafanyabiashara wado wa mchele wafikiwa na viongozi wa Machinga jiji la Mbeya (picha na Ezra Mwilwa)

Utekelezaji wa Maagizo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suruhu Hassan kuwapatia wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga vitambulisho maalumu waanza kutekelezaji.

Na Ezra Mwilwa

Umoja wa wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga jiji la Mbeya wakiongozwa na Mwenyekiti wa Machinga Jiji Ndg. Waziri Hemed wamewatembelea wafanyabiashara wa soko la Ikuti Iyunga jijini Mbeya kuelimisha juu ya usajili wa kupata kitambulisho cha mjasiriamali.

Akizungumza na wafanyabiashara hao mwenyekiti wa umoja huo ndg Waziri Hemed amesema kama wafanyabiashara ni muhimu kupata kitambulisho hicho ili kuepuka changamoto mbalimbali za ulipaji kodi.

Mwenyekiti wa Umoja wa Machinga jiji la Mbeya ndugu Waziri Hemed akiendelea na utoaji wa kwa wajasiliamali(picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya mwenyekiti wa Machinga jiji la Mbeya

Kwaupande wake Afisa Mendeleo wa kata ya Iyunga Selina Mwakifuna amesema kutokana na mfumo wa kujaza taarifa za mhusika kwanjia ya Fomu inasaidia kukamilisha zoezi kwa urahisi na uharaka zaidi.

Afisa Maendeleo kata ya Iyunga Selina Mwakifuna (picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya Afisa Maendeleo kata ya Iyunga

Nao baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Ikuti Iyunga wamesema wamepokea kwa furaha ujio wa kitambulisho cha mjasiliamali pia wameiomba serikali iharakishe zoezi hilo.

Baadhi ya wafanyabiashara soko la Ikuti kata ya Iyunga jijini Mbeya (picha na Ezra Mwilwa)
Sauti za baadhi ya wafanya biashara soko la Ikuti kata ya Iyunga Jijini Mbeya