Baraka FM

Moravian Vwawa yaungana na wakristo duniani kuadhimisha sikukuu ya pentecost

19 May 2024, 09:09

Katibu mkuu mstaafu Jimbo la Mbozi na Kiongozi wa ibada ya Pentecost hapa ushirikani Vwawa Mch.Sositen Mwasenga(picha na Hobokela Lwinga)

Dunia leo kupitia imani ya kikristo inaadhimisha ibada ya Pentecost,siku ambayo inasifika kwa waumini kuvaa mavazi meupe.

Na Hobokela Lwinga

Kanisa la Moravian Tanzania limeungana na waumini wengine duniani kuadhimisha ibada ya siku ya pentecost.

Pentecost kwa imani ya kikristo ina maana kubwa kwani ni siku ambayo Mungu alimwachilia Roho Mtakatifu kwa ajili ya maongozo ya kiroho.

Baadhi ya waumini wa kanisa la Moravian Ushirika wa Vwawa wakimwabudu Mungu katika ibada ya Pentecost (picha na Hobokela Lwinga)

Katika siku hii muhimu katika imani ya kikristo baraka fm imeshiriki ibada hii na kurusha mbashara kutokea katika kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Mbozi Ushirika wa Vwawa mkoani songwe.

Kwaya ya Vijana kati (Agano choir)wakiimba wimbo wenye maudhui ya Pentecost (picha na Hobokela Lwinga).

Katika ibada hii waumini wa kanisa hili wameendelea kumtukuza Mungu na kutoa ushuhuda wa namna ambavyo Mungu amewatendea.