Wanawake jitokezeni kupata mafunzo ya kujenga ndoa zenu
3 May 2024, 09:48
Kutokana na utandawazi kuendelea kukua katika ulimwengu huu wanawake wametakiwa kujitokeza katika semina mbalimbali kujifunza namna bora ya kuishi kwenye ndoa zao.
Na Iman Anyigulile
Wanawake mkoani Mbeya wametakiwa kujifunza mara kwa mara mafundisho ya ndoa ili kuweza kuimarisha ndoa zao na kujari familia zao.
Hayo yameleezwa na mchungaji Prisca Mwasansu wakati alipokuwa akizungumza kwenye kongamano la wanawake lililofanyika katika kanisa la RGC Victori mji mdogo wa Mbalizi mkoani Mbeya.
Mch Mwasansu amesema kuwa mwanamke anatakiwa kuwa na uwezo wa kufikiri , kuamua na kutenda lengo ni kupata watu walio sahihi katika nyanja mbalimbali kwenye jamii.
kwa upande wao wanawake walioweza kuhudhuria kongamano hilo wamesema kuwa kupitia kongamano hilo wamejifunza namna bora ya kuwa na uvumilivu katika ndoa na mwanamke kuwa jasiri na kiungo katika familia.