CHADEMA Mbeya yachagua viongozi, Masaga ambwaga Mwasote
9 April 2024, 13:28
Mabadiliko ni sehemu ya maisha ya binadamu hivyo ndivyo unaweza kusema hata kwenye taasisi kunahitaji mabadiliko ili kwenda mbele zaidi na kuyafikia mafanikio.
NA Imani Anyigulile
Wananchama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo mkoa wa Mbeya wamechagua viongozi mbalimbali wa ngazi ya mkoa, viongozi watakaosimamia miaka mitano kwenye chama chao.
Katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa Mfikemo jijini Mbeya CHADEMA imemchagua Masaga Pius Karol kuwa mwenyekiti wa mkoa, nafasi ambayo awali ilikua ikishikiliwa na Joseph Mwasote huku katibu wa chama hicho akichaguliwa Bw. Hamadi Mbeyale ambaye alikuwa akitetea nafasi hiyo.
Katika nafasi nyingine CHADEMA imemchagua John Mwambigija kuwa mwenyekiti wa baraza la wazee Chadema mkoa, Rehema Makoga kuwa katibu baraza la wazee, Elizabeth Mwakimomo kuwa mwenyekiti baraza la wanawake BAWACHA, huku Ruth Ngondo akichaguliwa kuwa katibu wa baraza la wanawake la chama hicho.
Viongozi wengine ni Elisha Chonya amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la vijana BAVICHA,na Ambokile Mwangosi kuwa katibu Baraza Hilo.
Baada ya uchaguzi huo mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa mbeya Masaga Pius Kaloli amewashukuru wapiga kura na washindani wake huku akiahidi kukisimamia chama kikamilifu.