Baraka fm yapongezwa kwa urushaji wa matangazo yenye tija kwa jamii
31 March 2024, 12:17
Redio Baraka ni redio inayomilikiwa na Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi,redio hii ndiyo redio ya kwanza ya dini iliyoanza kurusha matangazo yake na tangu ianze kurusha matangazo kumekuwa na shuhuda mbalimbali kutoka kwa wasikilizaji wake namna vipindi vinarusha ambavyo vimekuwa msaada kwao.
Na Hobokela Lwinga
Katibu mkuu mkoa wa Mbeya na naibu Katibu mkuu taifa wa N.L.C Mwinjilisti Willy Liberty Ngailo ameishukru redio Baraka kwa kutoa huduma za kiroho katika matangazo yao ambayo yamekuwa sehemu ya mafanikio ya huduma ya New Life In Christ (N.L.C)mkoa wa Mbeya.
Shukrani hizo amezitoa wakati akihubiri katika ibada ya Pasaka iliyofanyika katika kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Saza mkoani Songwe
Mwinjilisti Ngailo ametaja baadhi ya kazi ambazo ambazo kituo cha redio Baraka kimekuwa kikifanya ikiwemo kurusha matangazo ya huduma hiyo katika ibada ya kupanda na kuvuna ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka Jijini Mbeya.
Sambamba na hayo amewataka waumini kutokuwa waigizaji katika kumtumikia Mungu badala yake wanatakiwa kumtafuta Mungu na kuishi maisha Matakatifu.
Kwa upande wake mchungaji wa kanisa la Moravian Ushirika wa Saza Enedri Mwashibale amesema radio baraka ni chombo cha Kanisa la Moravian hivyo kila mshirika anapaswa kujivunia na kuwa sehemu ya kuwezesha kurusha matangazo kwa kutoa sadaka.
Hata hivyo baadhi ya waumini wamefurahia uwepo wa redio baraka kufika ushirikani kwao huku wakisema kituo hicho kimekuwa msaada mkubwa katika kutoa elimu ya Kiroho na Kimwili.