Imarisheni ulinzi kwenye maeneo yenu
27 March 2024, 11:22
Jukumu la ulinzi ni la kila mtu kwenye eneo lake na ulinzi wa jamii unatajwa kuwa chanzo cha kuimarisha amani kwani matukio mengi yamekuwa yakifichuliwa na wananchi.
Na Imani Anyigulile
Vijana wa mtaa wa kabwe na bank kata ya Ruanda jijini Mbeya wameombwa kushirikiana kwa pamoja kufanya ulinzi shirikishi ili kuweza kuzuia uharifu unaofanywa na baadhi ya watu ndani ya mitaa.
Hayo yamesemwa na afisa polisi ASP Nuru Mahenge wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wa Kabwe mkutano ambao umelenga kujadili suala la ulinzi na usalama ndani ya mitaa.
Inspeta Mahenge amesema kuwa vijana wanatakiwa kujipanga kufanya doria za alfajiri na jioni ili kuweza kuwakamata watu wanaohusika kufanya uharifu.
Kwa upande wake polisi mkaguzi wa kata Ruanda jijini Mbeya Ispecta Fatma Hamdan amewaomba wazazi na walezi kuwaepusha watoto wao na makundi mabaya ambayo yanaweza kumsababishia mtoto kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinisia.
Nao wenyeviti wa mtaa wa kabwe na mtaa wa bank George Mwandago na Anyamwile Mwasaga wamewataka wazazi kukaa na watoto wao na kuwakanya kuhusu suala la uharifu unaofanyika ndani ya mitaa hiyo.
Hata hivyo wananchi wa mtaa wa kabwe na mtaa wa bank wameliomba jeshi la polisi kuwaondolea watoto wa mitaani wanaopatikana eneo la soko la SIDO na stand ya kabwe ambao wamekua chanzo cha uharifu.