Wakristo mtumikieni Mungu katika maisha yenu yote hapa duniani
26 March 2024, 10:34
Kwaresma kwa mkristo ni nguzo ya imani na inakumbusha mateso ya Yesu Kristo katika kipindi hiki waumini wanaaswa kufanya matendo mataua(matakatifu) ikiwa ni pamoja na kufanya matendo ya upendo na amani.
Na Iman Anyigulile
Waumini wa dini ya kikristo nchini wametakiwa kusoma maandiko ya biblia na kuweza kuyatafakari kwa kina hasa katika kipinidi hiki cha kusheherekea sikukuu ya pasaka.
Hayo yameelezwa na Mch. Ekisa Shibanda ambae ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Teku wakati akizungumza na kituo hiki juu ya umuhimu wa ibada ya mitende iliyofanyika kanisa la Moravain ushirika wa Teku jijini Mbeya.
Kwa upande wake Mchungaji Mery Kategile ambae ni Mhadhiri wa chuo cha Teku idara ya theologia amesema wakristo wanatakiwa kuishi maisha ya kumcha Mungu, upendo na Amani.
Nae katibu wa kanisa la Moravian ushirika wa Teku Aines Mpalanzi amewaomba wakristo kuacha kwenda kanisani kwa mazoea badala yake wawe wafuatiliaji wa maandiko ya biblia.