10 wakamatwa wakitorosha kilo 9.8 za dhahabu mkoani Mbeya
19 March 2024, 18:42
Shughuli za kila mwanadamu zinatengemea kufanywa kupitia taratibu na sheria za nchi,na endapo mtu akikiuka hayo ni lazima achukuliwe hatua kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.
Na Hobokela Lwinga
Watu 10 wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kutorosha vipande 334 vya dhabu iliyochomwa yenye uzito wa kilogramu 9.5 ambayo inaghalimu kiasi Cha fedha za kitanzania zaidi ya shilingi bilioni moja.
Akitoa taarifa kwa wanahabari jijini mbeya waziri wa madini Anthony Mavunde amesema watuhumiwa hao walikamwatwa machi 16 mwaka huu mtaa wa Ilomba na kata ya ilomba jijini mbeya wakiwa na vifaa vya kuchomea dhahabu na mizani ya kupimia pamoja na Sawa za kusafishia ambapo uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Mavunde amesema tukio hili ni la pili kutokea Mkoani Mbeya na kuagiza kamishina wa madini kuzifuta leseni zote zinazomilikwa na watu hao pamoja na leseni zote zinazomilikea na watu hao nje ya Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mrakibu mwandamizi wa uhamiaji Mbarack Alhaji Batenga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya amesema ili kukomesha uhalifu unaofanywa na baadhi ya watu kwenye mitaa viongozi wa mitaa
Hata hivyo Kamanda wa Polisi ACP Benjamini Kuzaga amesema wao kama jeshi la polisi wataendelea kukabiliana na wahalifu wote wanaokiuka taratibu na sheria za nchi.