Mradi wa Dream kuwanufaisha wasichana Mbeya, Songwe
18 March 2024, 12:24
Katika dunia ya sasa kundi la wasichana wanapaswa kulindwa na kupewa mazingira mazuri ambayo yatawafanya kuondokana na changamoto zinazowakabili.
Na mwandishi wetu
Shirika la kimataifa la HJFMRI limesema linatarajia kutoa Sh 500 milioni kuwezesha mabinti balehe na wasichana vijana kupitia mradi wa dreams kwa ufadhili wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR).
Mkurugenzi Mkuu wa HJFMRI Tanzania, Sally Chalamila amesema hayo Machi 16 mwaka huu wilayani Kyela wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali na mashine za kisasa vyenye thamani ya Sh 178 milioni.
Mashine na vifaa hivyo vimetolewa na Shirika la HJFMRI kupitia WRAIR-DOD kwa ufadhiri wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani (PEPFAR) kwa kushirikiana