Hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya kusaidia vijana wabunifu wenye ulemavu
8 March 2024, 08:31
Na Ezekiel Kamanga
Mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji amesema hospitali iko tayari kusaidia kijana yeyote mwenye ubunifu kwa mambo yanayogusa sekta ya afya kwa ustawi wa jamii bila kujali ni mfanyakazi wa hospitali, kwani kijana yoyote atakayefanikisha ubunifu huo sifa ni kwa nchi (Tanzania) na maslahi mapana kwa wananchi wote.
Dkt. Mbwanji ameyasema hayo leo baada ya kukutana ofisini kwake na kijana Augustine Erasto Njowoka Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Technolojia Mbeya (MUST) aliyeonesha nia ya kutengeneza fimbo maalum anayotumia mtu asiyeona yenye uwezo wa kutambua vikwazo vilivyoko mbele kama vile jiwe, chuma, mashimo pamoja na madimbwi ya maji kwa kupiga alamu na mtetemo (vibration) kama ishara.
kwa upande wake mbunifu Augustine Erasto Njowoka Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Technolojia Mbeya (MUST) amesema aliona watu wasiona wanachanagamoto nyingi hali hiyo ndiyo iliyomshawishi yeye kuingia kwenye ubunifu wa kutengeneza fimbo zenye uwezo wa kutambua vikwazo wanavyokutana navyo wakati wa kutembea.
Katika hatua nyingine viongozi wa hosiptali wameuunga mkono juhudi za Ndugu Augustine kwa kumnunulia kopmyuta mpakato(Laptop) kwaajili ya kumwezesha katika kufanikisha malengo yake ambapo baada ya kukamilisha maboresho ya utengenezaji wa fimbo hiyo vilevile anategemea kutengeneza miwani inayotumia akili bandia (artificial intelligence) yenye uwezo kutambua vitu vinavyomzunguka katika mazingira yake kwa kuvitaja majina.