Diwani Mariam:Wawepo wataalamu wa saikolojia kwenye kata
7 March 2024, 15:57
Mamilioni ya watanzania wanajihususha na ujasiriamali mdogo hali inayo wafanya wajiingizie kipato kutokana na hilo hawana budii kupata elimu inayowawezesha kufanya shughuli zao kwa weledi.
Na Hobokela Lwinga
Kuelekea kilele cha siku ya mwanamke duniani,diwani wa viti maalum jiji la Mbeya Mariam Jason ameshauri kuwepo na wataalamu wa saikolojia kuanzia ngazi ya kata ili kuondoa au kupunguza matatizo ya magonjwa ya akili yanayoikabili jamii.
Ushauri huo ameutoa akiwa mgeni rasmi katika semina ya ujasiriamali iliyoandaliwa na kampuni ya mama kansolele products iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha maendeleo ya jamii uyole jijini Mbeya.
Wakati akifundisha kwenye semina hiyo msaikolojia kutoka hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya Yisambi Mbuwi Ndagamsu amesema unapofanya biashara yoyote unapaswa kuwa na nidhamu ya fedha.
Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi mkurugenzi wa Mama Kansolele Products Hamisa Abdalah Juma amesema lengo la semina ambazo wanaziandaa zinalengo la kumsaidia kila mtu kukua kiuchumi.
Baadhi ya washiriki katika semina hiyo wamesema wajasiriamali wanatakiwa kuwa wabunifu kwenye shughuli zao wanazofanya za kuwaingizia kipato huku wakiwashukru waandaaji wa semina hiyo.
Kauli Ya Siku Ya Mwanamke Duniani Inasema “Wekeza Kwa Mwanamke Kuharakisha Maendeleo Ya Taifa“