Chunya yavuka malengo zoezi la chanjo ya surua rubella
21 February 2024, 15:08
Na mwandishi wetu
Halmashauri ya wilaya ya Chunya imetoa chanjo ya Surua Rubella kwa watoto 44,942 sawa na asilimia 116.37 wakati lengo lilikuwa kuwafikia watoto 38,619 na kwa takwimu hiyo Halmashauri ya wilaya ya Chunya imekuwa ni wilaya iliyochanja watoto wengi kuliko wilaya nyingine yoyote ya Mkoa wa Mbeya ukilinganisha na malengo yaliyokuwa yamewekwa awali.
Akitoa taarifa ya zoezi kwa ujumla mratibu wa Huduma za Chanjo Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndugu, Blasio Kabwebwe amesema halmashauri ya wilaya ya Chunya ni kati ya wilaya Ngumu kuwafikia wananchi katika maeneo yao kwani kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kuna umbali mrefu lakini juhudi, kujituma na hata moyo wa uzalendo wa maafisa wanaohusika na zoezi la Chanjo ndiyo msingi wa kufikia lengo na hata kuvuka kiwango kama takwimu zinavyoeleza
“Kuwafikia wananchi wa Chunya kwa kiwango hicho sio kazi ndogo maana wilaya ya Chunya inajulikana wazi kwa jiografia yake lakini lazima nipongeze kazi kubwa inayofanywa na wataalamu ambao wamehusika katika zoezi la Chanjo, wamejituma sana na kwa moyowa uzalendo na matokeo yake ndo hayo katika mkoa tumefanya vizuri kuliko wilaya nyingine.