Ubovu wa magari wasababisha kuzorota kwa huduma za afya kwa wananchi Mbeya
14 February 2024, 21:16
Na mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Homera amewataka Madreva wa Magari ya Serikali kuyatunza Vyema na kujiepusha na Matumizi mabovu ya Barabara ikiwemo Kutembea Mwendo Mkali na kutojali alama za Barabarani Hali inayolelekea Ajali zisizo na Ulazima.
Leo Juma Tano Agosti 14 2024 katika Hafla fupi ya kuzindua na Kukabidhi Magari 14,Nane ya Wagonjwa na Sita ya Wasimamizi ambayo imefanyika Kata ya Nsalala Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Homera ameweka Wazi kuwa Ubovu wa Magari unasababisha kudhorota kwa Huduma za Afya kwa Wananchi kwa Kushindwa kuwafikisha sehemu za Kupewa huduma hasa wapatwapo na Changamoto.
Tukio hilo la kukabidhi Magari yatakayofanya Kazi Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya, RC Homera amelifanya kwaniaba ya Waziri Wa TAMISEMI Mh: Mohammed Mchengerwa.