Wawili wanusurika ajalini Mikumi wakielekea kwenye kipaimara
5 January 2024, 23:01
Na Hobokela Lwinga
Gari Aina ya gari Noah Yenye namba za usajili T507 DPP mali ya mchungaji James Mwakalile ambalo lilikuwa likifanya kazi katika misheni ya Morogoro imepata ajali katika eneo la karibu na kambi ya jeshi December 22,2023 .
katika gari hiyo kulikuwa na Dereva Elihuruma Lwinga ambaye alikuwa akimuendesha Mke wa Mwenyekiti wa Eneo la Misheni Morogoro Mrs James Mwakalile (MAMA KAJINGA) ambao walikuwa wakielekea kanisa la Moravian ushirika mang’ula kwenye ibada ya kipaimara December 24,2023 na wote walitoka salama katika ajali hiyo.
Mmoja ya manusura wa ajali hiyo ambaye ni Dereva amesema walipofika Mikumi Mbele ya Kambi ya Jeshi Mikumi tairi la kushoto la mbele lilipasuka ndipo gari lilikosa mwelekeo na kwenda pembeni hali iliyomfanya afunge breki na hapohapo gari ilianza kupinduka mara 3 kwenda chini ya Daraja na kudumbukia mtoni(mto Ruaha)ilikua saa 1 kasoro 10 usiku.
Amesema chini ya Daraja wakafanya utaratibu wa kutoka ambapo mama mchungaji James Mwakalile alifanikiwa kumfungua mkanda na kisha akatoka, na baada ya kutoka ndipo naye akafanya utaratibu wa kumtoa mama huyo kwenye gari.
Hata hivyo ameongeza kuwa licha ya kwamba kwenye gari kuliku na vitu vingi vikiwemo vyombo vya udongo vyote vilitoka salama isipokuwa dereva huyo alipoteza simu moja ambayo ilidumbukia kwenye maji.
Aidha amesema katika eneo la ajali ilikuwa ngumu watu kutambua kutokana na eneo hilo kuwa poli hivyo ilimfanya atafute njia ya kutokea kwa kupanda iliko barabara ili kupata msaada kwa watu wanaotembea barabarani wakiwemo bodaboda ambapo alifanikiwa na kuwaagiza kupeleka taarifa jeshini kwani ndio ilikuwa jirani zaidi.
amesema Muda mfupi wanajeshi 3 walikuja na kutoa msaada na ushirikiano wa kuzitaarifu mamlaka zingine ikiwemo polisi ambao walifika eneo la tukio.
Elihuruma Amesema Baadaye alikuja wachungaji wa Mikumi na Mangula na baadhi ya waumini wa kanisa la Moravian huku mch. James Mwakalile ambaye ni mume mama manusura Alikuja usiku huo na kisha safari ikaendelea kwenda mang’ula ambako kulikuwa na ibada ya kipaimara December 24,2023.