Madiwani Wilaya ya Kyela watembelea vivutio vya utalii wilayani Rungwe Mbeya
28 December 2023, 18:13
Na Hobokela Lwinga
Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mhe January Mwakasege (Mwenye suti nyeusi )amewaongoza Madiwani kutoka Wilaya ya Kyela kutembelea vivutio vya Utalii mbalimbali vinavyopatikana wilayani Rungwe.
Madiwani kutoka Kyela wamefanya ziara hii ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani na kujifunza fursa mbalimbali za Uwekezaji zinazopatikana katika wilaya ya Rungwe.
Baadhi ya maeneo ya vivutio vilivyotembelewa ni pamoja na daraja la Mungu pamoja Kinjungu vyote vinapatikana katika mto Kiwira kata ya Lupepo .
Madiwani wamejionea fursa mbalimbali zilizopo na kuhamasishwa wageni wengine kujitokeza kuja na kujionea namna Rungwe ilivyobahatika kuwa maeneo mazuri na mwanana kwa utalii.
Katika Mwaka huu wa fedha 2023/24 Rungwe imebahatika kutembelewa na wageni (Utalii) kutoka Halmashauri mbalimbali ikiwemo Kutoka Unguja na Sikonge Tabora.
Kwa wastani kwa mwaka Halmashauri ya Rungwe hupokea watalii wapatao 4500 na hivyo kusaidia kuongeza pato la Serikali kwa kulipa tozo mbalimbali, huduma ya malazi na chakula, pato kwa wapiga picha, huduma ya usafiri na mengine mengi.