Kayange: Viongozi wa maji wanaozuia wananchi kutoa kero wachukuliwe hatua
8 November 2023, 13:47
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya imewaomba watumiaji wa maji kulipa ankara zao kwa wakati ili mamlaka hiyo iweze kujiendesha na kutoa huduma kwa ufanisi.
Na Sifael Kyonjola
Akizungumza na kituo hiki mkurugenzi wa mamlaka hiyo CPA Gilbert Kayange amesema kuwa mamlaka hiyo haitegemei ruzuku kutoka serikalini hivyo ni muhimu wananchi walipe malipo yao.
Ameongeza kuwa mamlaka ya maji imeanza kutoa mita za luku za maji kwa makampuni makubwa ili watumiaji walipe kulingana na matumizi yao huku akisisitiza kuwa mchakato huo utawafikia wananchi wote.
Katika hatua nyingine amemtaka mkurugenzi wa maji katika mji wa Mbalizi GEORGE ALBANO kuwachukulia hatua baadhi ya watumishi wanaozuia wananchi kufikisha kero zao kwa viongozi wa mamlaka hiyo ili hatua zichukuliwe