Bilioni 5 zawanufaisha wananchi ujenzi mradi wa maji Mbarali
5 October 2023, 20:35
Maji ambayo imekuwa ikitajwa kuleta migogoro ya kindoa, kwa ujumla kero hiyo imekuwa ikitatuliwa pindi ambapo mamlaka yenye wajibu wa kupeleka huduma inapopeleka eneo husika, huku wajibu wa kutunza mradi huo likibaki wa watumiaji ambao ni wananchi.
Na mwandishi wetu
Serikali imewezesha ujenzi wa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 5 unaosimamiwa na RUWASA katika kata ya Mawindi halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe.Juma Zuberi Homera amewataka wananchi kutunza miundombinu ya mradi huo ili uendelee kutoa huduma na kuwapunguzia kero ya kufuata maji umbali mrefu.
Mradi huo utahudumia vijiji vitano vinavyopatikana ndani ya kata ya Mawindi ambapo vijiji hivyo ni Itipingi, Manienga, Matemela, Mkandami na Ipwani.
RC Homera ameanza ziara rasmi ya kuzitembelea halmashauri zote za mkoa wa Mbeya ili kukagua miradi, kufanya mikutano ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.