Umeme waleta mgao wa maji mkoani Mbeya
13 September 2023, 18:43
Maji ni uhai, viumbe wote hai wanategemea maji hata nje ya viumbe hai bado kumekuwa na uhitaji wa maji,nchi ya Tanzania imekuwa ikitegemea maji kuzalisha nishati ya umeme hivyo maji ni kila kitu kwenye shughuli yoyote ya binadamu.
Na Hobokela Lwinga
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya(WSSA)imekri kuwepo kwa mgao wa maji chanzo kikitajwa kuwa ni upungufu wa maji kwenye vyanzo vya kuzalishia maji pamoja na kukatika katika kwa umeme.
Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya Neema Stantony wakati akieleza namna ambavyo mamlaka hiyo inavyofanya kazi kipindi hiki ambacho nchi inakabiliwa na tatizo la kukatikakatika kwa umeme.
Bi,Neema amesema kama mamlaka inafanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa kila mwananchi wakati wote sambamba na hayo afisa huyo amewashauri wananchi kuhifadhi maji kwenye vyombo pindi yanapopatikana kutokana na zamu zinazotolewa na mamlaka hiyo.
Nao baadhi ya watumiaji wa maji ambao ni wakazi wa mbeya wameeleza namna ambavyo kero ya maji imekuwa ikiwaathiriambapo wamesema maji hayo yamekuwa yakitoka kwa mgao iwe kijijini au mjini.
Mkoa Wa Mbeya Ili Uweze Kukidhi Mahitaji Ya Maji Kwa Wananchi wake Unahitaji Angalau Lita milioni 90 ambapo kwa sasa mamlaka hiyo inazalisha maji lita milioni 66.6 kila siku.