Baraka FM
Baraka FM
5 October 2025, 11:45

kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29,Oktoba 2025 viongozi wa dini wameendelea kuhimiza waumini kuombea taifa ili kuvuka salama.
Na Ezekiel Kamanga
Mchungaji Nelson Mwaisango Mwenyekiti pia Katibu mstaafu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini amewataka waumini wa Kanisa la Moravian Tanzania kuombea amani nchini hasa kipindi hiki cha uchaguzi ili waendelee kulitangaza neno la Mungu bila vikwazo.

Mchungaji Mwaisango ameyasema hayo katika ibada iliyofanyika Ushirika wa Nyibuko lililopo Kijiji cha Syukula Kata ya Kimo Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Amesema nchi nyingine hushindwa kumuabudu Mungu kutokana na vita vilivyopo katika nchi zao hivyo kila muumini atenge muda wa kuiombea amani nchi yetu na Kanisa kwa ujumla.
