Baraka FM
Baraka FM
1 September 2025, 19:39

Vitabu vya dini vinatuasa kuishi maisha ya kusaidia wengine kwani hakuna ambaye aliumbwa kwa mategemeo ya kukumbana na changamoto duniani.
Na Hobokela Lwinga
Kituo cha Redio Baraka kinachomilikiwa na kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi kimewashukru wadau wake wote kwa kutoa ushirikiano kufanikisha zoezi la kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wafungwa wa gereza la wilaya ya ileje mkoani Songwe.
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo,kaimu meneja wa kituo cha Redio Baraka chenye makao makuu yake mkoani Mbeya ndugu Sifael Kyonjola amesema lengo lilikuwa limekusudiwa limetimia.

Aidha mwenyekiti wa wadau bw.Christopher Sengo amesema wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na chakula, mashine za kunyolea,sabuni,mafuta pamoja na sukari.

Kwa upande wake mchungaji kutoka idara ya magereza kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Stephano Ngondya amesema kila mtu anawajibu wa kutoa msaada kwa wahitaji.

Baadhi ya washiriki waliofika katika gereza la wilaya ya Ileje mkoani Songwe wamesema wao wameteleza wajibu wa kusaidia wahitaji kama ambavyo Mungu anavyoagiza kupitia Biblia Takatifu.

Kituo hiki cha cha Redio Baraka kwa kushirikiana na wadau wake kimekuwa na utaratibu wa kila mwaka kuyaona na kutoa misaada kwa makundi mbalimbali ikiwemo, wazee, yatima na kutembelea wafungwa walioko magerezani
