Baraka FM

TAKUKURU Mbeya yaokoa milioni 47 mikopo ya halmashauri

19 August 2025, 19:23

Makao makuu ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya (picha na Hobokela Lwinga)

Kwa kutoa taarifa ya vitendo vya rushwa, wananchi wametakiwa kuwasilisha taarifa hizo katika ofisi za TAKUKURU za mkoa na wilaya au kupiga simu bure 113.

Na Hobokela Lwinga

TAKUKURU mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuokoa Zaidi ya shilingi milioni 47 katika halmashauri ya wilaya ya Mbarali na kuiwezesha halmashauri hiyo kuongezeka kimapato kwa zaidi ya shilingi milioni 200.

‎Akitoa taarifa kwa vyote vya habari kwa mwezi April hadi juni 2025, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya Maghela Ndimbo amesema fedha hizo zilizookolewa zilitokana na mkopo wa asimilia 10 unaotokana na halmashauri unaolenga makundi ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

‎Aidha katika ufuatiliaji wa miradi ya elimu,barabara afya na miundombinu TAKUKURU ilibaini uwepo wa mtunza vifaa asiye sifa katika mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya amali usoho muungano wenye thamani ya bilion moja na milioni mia sita unaotekelezwa katika halmashauri ya wilaya Mbeya.

‎Katika hatua nyingine TAKUKURU imeokoa zaidi ya shilingi milioni 17 ambazo ni fedha za wanafunzi wa chuo kikuu cha sayansi na tekinolojia Mbeya MUST ambazo zilikuwa zinadaiwa na wanafunzi 51 walizolipa zaidi kipindi wakiwa wanasoma chuoni hapo.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya Maghela Ndimbo(picha na Hobokela Lwinga)

‎Sanjari na hayo Maghela amesema TAKUKURU imeendelea kutoa elimu kwenye makundi mbalimbali ikiwemo kutoa elimu ya program ya TAKUKURU rafiki kwa zaidi ya kata 14 na kufanya uimarishaji wa klabu 61,semina 34, mikutano ya 36,makala 6 ,vipindi 4 pamoja na moenesho 2.

‎Mkuu huyo amewataka wananchi kujiepusha na vitendo vya rushwa na kushiriki kikamilifu katika kuzuia vitendo vya rushwa katika maeneo yao hasa kuelekea katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika October 29,mwaka huu.