Baraka FM

Askofu Pangani awataka waumini kuwana ushirikiano

5 August 2025, 06:50

Askofu Pangana na Mch. Johannes Crame(picha Hobokela Lwinga)

kutokana na ushirikiano wa kanisa la Moravian Tanzania kuwa naushikiano na mataifa mengine katika kuhudumua kanisa waumini wametakiwa kutoa ushirikiano kwa watumishi wanao toka nchi za nje na ndani.

Na Ezra Mwilwa

Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi Robert Pangani amelitaka kanisa kuwa na umoja ili kuifanya Injili kuenezwa kila mahali.

‎Rai hiyo imeitoa kwenye ibada maalumu ya kumuaga mtumishi wa Mungu mchungaji Johannes Crame kutoka katika kanisa la st.Gallen La nchini uswisi aliyemaliza muda wake wa umeshonari nchini Tanzania katika kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi.

Sauti ya Askofu Robert Pangani

‎Aidha askofu Pangani amewataka wakristo kuachana na tabia ya utengano badala yake waonyeshe upendo kwa kila mtu wanayrkutana nayo.

Baadhi ya watumishi wa kanisa(picha na Hobokela Lwinga)

Katika hatua nyingine amemwelezea mchungaji Johannes Crame kuwa msaada mkubwa katika kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya kanisa kwa takribani miaka kumi na tano.

Sauti ya Askofu Pangani

kwaupande wake Mch Johannes Crame amesema kwakipindi cha miamka kumi na Tano ya huduma ndani ya kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi amejifunza mambo mengi kama vile kuhubiri neno la Mungu kwa matendo kwa kuhudumua yatina, wajane na watu wanao ishi katika mazingira magumu.

Mch Johannes Crame(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Mch Johannes Crame