Baraka FM

Madereva Nyanda za Juu Kusini wagoma, faini za barabarani zatajwa

20 June 2025, 12:15

Baadhi ya magari ya abiria yakiwa yamepaki katika stand ya mpemba, Momba mkoani Songwe (picha ya mwandishi wetu)

Mapema leo katika barabarani ya Tanzania, Zambia hali imekuwa mbaya kwa abiria baada ya madereva wanaotumia njia hiyo kusafirisha abiria kugoma kufanya kazi.‎‎

Na Mwandishi wetu,Songwe‎‎

Madereva wanaofanya safari zao Mbeya,Ileje mkoani Songwe na sumbawanga mkoani Rukwa wamegoma kwa kushinikiza mamlaka za usimamizi wa sheria za barabarani yaani traffic kuacha tabia ya kuchukua fedha zao bila utaratibu.‎‎

Mgomo huo umeanza mapema leo June 20,2025 asubuhi katika standi ya mpemba iliyopo katika mji wa Tunduma wilaya ya Momba mkoani Songwe.‎‎

Baadhi ya madereva hao wamesema barabarani kumekuwa na utaratibu wa hovyo wa faini zisizofuata utaratibu.

‎‎Aidha mwenyekiti wa madereva hao mkoa wa Songwe Tandi Kibona amesema mwafaka bado haujapatikana huku akisema wao kama viongozi wanawasikiliza wanachama wao kile wanachokihitaji.‎‎

Mwenyekiti wa madereva hao mkoa wa Songwe Tandi Kibona(picha na mwandishi wetu)

Baadhi ya abiria walioshindwa kusafiri kutokana na mgomo huo wameziomba mamlaka zinazohusika kuwasaidia ili waweze kusafiri.

Baadhi ya abiria wakiwa standi ya Mpemba huku wakiwa wamekosa la kufanya (picha na mwandishi wetu)

Jitihada za kuzitafuta mamlaka zinazohusika zinaendelea ili kujua hatma ya jambo Hilo.