Baraka FM

Somabiblia wawatoa msaada kwa wahitaji

14 June 2025, 15:46

Baadhi ya Askari magereza na wawakilishi wa soma Biblia( picha na Ezra Mwilwa)

Kampuni ya soma Biblia imefikisha miaka kumi katika kuadhimisha miaka hiyo wametembelea jeshi la magereza Rwanda Mbeya kuwatazama wafungwa na kutoa msaada wa vitu mbalimbli.

Na Ezra Mwilwa

Wadau na taasisi mbalimbali wameombwa kutowatenga wahitaji badala yake wanatakiwa kujenga utamaduni wa kuwatembelea na kuwasaidia wahitaji misaada mbalimbali kwani kufanya hivyo ni sadaka na  thawabu mbele za Mungu.

Ombi hilo limetolewa na Meneja wa Shirika la SomaBiblia Mkoa wa Mbeya Ndg. Agrey Polepole wakati shirika hilo lilipo tembelea kutoa msaada wa mahitaji ya kiroho na kijamii kwa wafungwa na mahabusu katika Gereza la Ruanda lilipo Mkoani Mbeya ikiwa ni maadhimisho ya miaka 10 ya utoaji wa huduma ya injili na udiakonia kwa shirika hilo.

Meneja wa soma Biblia tawi la Mbeya kushoto akikabhi vitabu(picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya Meneja wa Shirika la SomaBiblia Mkoa wa Mbeya Ndg. Agrey Polepole

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa msaada huo wa vitabu vya Dini pamoja Chakula Mkuu wa Gereza hilo Christopher Fungo ametoa shukurani kwa shirika hilo akisema vifaa hivyo vitawasaidia wafungwa si kiafya tu bali na kiroho pia.

Mkuu wa jeshi la magereza Rwanda(wapili kulia) akitoa shukrani( picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya Mkuu wa Gereza hilo CPA Christopher Fungo

Nae Mchungaji Ambokile Mwanyiru kutoka kanisa la KKKT Usharika wa Sayuni ameeleza namna ushirikiano mkubwa unaotolewa na shirika hilo kwa kusambaza nakala mbalimbali za neno la Mungu ambazo ni nyenzo ya watu kukua kiimani huku akikumbusha kuwa ni jukumu la udiakoni ni la kila mmoja.

Sauti ya Mchungaji Ambokile Mwanyiru

Kwa upande wao wahudumu katika shirika hilo wameeleza namna wanavyo toa huduma kwa wahitaji kutoka mataifa mbalimbali huku wateja wanaopata huduma katika taasisi hiyo wakipongeza kwa ubora wa huduma zinazo tolewa na shirika hilo.