Baraka FM

Watu wenye ulemavu Songwe waja naombi

11 June 2025, 19:40

Baadhi ya watu wenye ulemavu wa miguu na mikono(picha na Ezra Mwilwa)

kutokana na kuwepo kwa mashindano ya watu wenye ulemavu ngazi ya Taifa timu wa walemavu mkoa wa Songwe wameomba wadau mbalimbli kuwaunga mkono ili waweze kushiriki mashindano hayo.

Na Ezra Mwilwa

Timu ya soka ya walemavu wanaume mkoani Songwe wameomba watumbalimbali kuwasaidia vifaa vya Michezo ili kuendeleza vipaji vyao.

Wachezaji hao wamesema wamekua wakipata changamoto ya vifaa vyamichezo kama mangongo na vifaa vitakavyo wawezesha kufanya vizuri katika michezo.

Baadhi ya watu wenye ulemavu(picha na Ezra Mwilwa)
Sauti za wachezaji

kwa upande wa Kocha wa kikosi hicho Charles Mwamlima amesema wanatamani kusaidiwa vifaa hivyo vitakavyo wasaidia katika mashindano .

Kocha Mwamlima wa timu ya watu wenye ulemavu mkoa wa Songwe (picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya kocha Mwamlima

Kocha Mwamlima amesema niwakati sahihi kwenda ngazi ya Mitaa, kata mpaka wilaya kitafuta vipaji kwa watu wenye ulemavyo nakushiriki mashindano ya Taifa yanayo tarajiwa kufanyika mwezi wa Saba mwaka huu

Sauti ya Mwamlima akieleza kutafuta vipaji