Baraka FM
Baraka FM
24 May 2025, 15:29

Kuelekea uchaguzi Mkuu October 2025 baadhi ya makada kupitia vyama vyao vya siasa wameanza kutangaza nia zao kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo udiwani,ubunge na urais.
Na Ezra Mwila
Kada wa chama cha mapinduzi na mwandishi wa habari mkoani Mbeya Charles Mwakipesile ametangaza rasmi kugombea jimbo la Mbeya mjini Pindi mchakato utakapotangazwa.
Kada huyo ametangaza dhamira yake wakati akizungumza na wanahabari jijini Mbeya,amesema endapo atapewa ridhaa hiyo ataendeleza mazuri yote aliyo yaanzisha mbunge aliyepo Dkt.Tulia ambaye ametangaza kugombea jimbo la Uyole baada ya kugawanywa.

Nao baadhi ya wananchi waliopo Jimbo la Mbeya mjini wamesema wanamshukuru Dkt Tulia kwa Utumishi wake hivyo wanaomba atakae pata nafasi ya kuongoza Jimbo Hilo aendeleze pale atakapoishia DKT Tulia Akson.

Jimbo la Mbeya mjini limegawanywa na kupatikana kwa jimbo la Uyole ambalo Dkt.Tulia ametangaza rasmi kugombea katika nafasi ya ubunge.