Baraka FM
Baraka FM
22 May 2025, 09:22

Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako mbalimbali ya kuwabaini wahalifu wa makosa mbalimbali.
Na Hobokela Lwinga
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mbeya Linawashikilia Watuhumiwa Wawili Wote Wanawake, Ambao Ni Seva Simwinga [29] Na Sara Simwinga [35] Wafanyabiashara Na Wakazi Wa Mponja Uyole Jijini Mbeya Kwa Tuhuma Za Kupatikana Na Shehena Ya Dawa Za Kulevya Aina Ya Bangi Yenye Uzito Wa Kilogram 320.
Akizungumzia Kukamatwa Kwa Watu Hao, Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga Amesema Watuhumiwa Walikamatwa Mei 21, 2025 Majira Ya Usiku Katika Operesheni Maalum Iliyofanywa Na Jeshi La Mkoa Huo Katika Mtaa Wa Mponja Uliopo Kata Ya Uyole, Tarafa Ya Iyunga Jijini Mbeya.
Kamanda Kuzaga Ameeleza Kuwa Watuhumiwa Hao Walikutwa Na Magunia 4 Na Masanduku 4 Yenye Dawa Hizo Za Kulevya Wakiwa Wamehifadhi Ndani Ya Nyumba Wanayoishi.
Katika Hatua Nyingine Kamanda Kuzaga Ameeleza Kuwa Pia Jeshi Hilo Linawashikilia Billy Mtafya [19] Fundi Magari, Mkazi Wa Uyole Jijini Mbeya Na Joseph Nyalusi [25] Kondakta Wa Basi, Mkazi Wa Dodoma Wakiwa Na Dawa Za Kulevya Aina Ya Bhangi Yenye Uzito Wa Kilogram 30.
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mbeya Kupitia Kamanda Benjamin Kuzaga, Limetoa Wito Kwa Baadhi Ya Wananchi Wanaojihusisha Na Biashara Haramu Ya Dawa Za Kulevya Kuacha Mara Moja Kwani Haina Nafasi Katika Jamii Na Kwamba Jeshi La Polisi Mkoani Humo Lipo Makini Kuwabaini Na Kuwakamata Wote Wanaojihusisha Na Biashara Hiyo.