Baraka FM

Mwenyekiti wa kitongoji adaiwa kufyeka mazao ya wananchi

19 March 2025, 08:11

Mchezo wakahawa ulio fyekwa(picha na Ezekiel Kamanga)

Kufuatia changamoto ya Barabara katika kitongoji cha Lwifwa Kijiji Cha lwifwa Kata ya Kisiba Halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe mwenyekiti adaiwa kufyeka mazao ya wananchi bila idhini yoyote.

Na Ezekiel Kamanga

Wananchi wa Kitongoji cha Lwifwa Kijiji Cha lwifwa Kata ya Kisiba Halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe wamemlalamikia Mwenyekiti wa Kitongoji Anyitike Mwakasege kwa tuhuma za kufyeka mazao na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni sitini kwa madai ya ujenzi wa barabara.

Charles Mwaipopo ni mmoja wa waathirika amesema miche yake hamsini na sita ya kahawa na kakao miche sita yenye thamani ya shilingi milioni ishirini imefyekwa na Mwenyekiti huyo huku wananchi wengine wakidai kupata hasara ya zaidi ya shilingi milioni arobaini.

Baadhi ya Miche ya kahawa inayo daiwa kufyeka(picha na Ezekiel Kamanga)

Ambwene Japheth ni Mwenyekiti wa Kijiji amedai hakupata taarifa yoyote ya zoezi hilo linalodaiwa ni la utengenezaji wa barabara.

Bi Natasha Kamwela Mtendaji wa Kitongoji cha Lwifwa amesema zaidi ya wananchi arobaini wamekatiwa mazao yao baada ya kupokea malalamiko alisitisha zoezi hilo huku akishangazwa na kitendo cha Mwenyekiti kuendesha zoezi hilo bila kumshirikisha na kwamba Mwenyekiti ametoroka baada ya sakata hilo.

Baadhi ya mazao yaliyo fyekwa kahawa na migomba(picha na Ezekiel Kamanga)

Diwani wa Kata ya Kisiba Ambakisye Mwakanyamale amekiri kupokea malalamiko kutoka kwa waathirika na kuwataka wananchi wawe watulivu wakati suala hili likishughulikiwa kisheria.

Baadhi ya Viongozi wamekuwa wakijifanya miungu watu kwa kujichukulia maamuzi bila kuwasilisha wananchi.Mpaka sasa haijafahamika Mwenyekiti huyo wa Kitongoji amejificha wapi kwa lengo la kukwepa mkondo wa sheria.