

18 March 2025, 20:07
Katika kuadhimisha wiki ya maji, Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mbeya UWSA imetoa ofa kwa wateja wake wenye malimbikizo ya ankara za maji kulipa nusu gharama na kisha kuwarejeshea huduma hiyo bure.
Na Ezra Mwilwa
Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa mamlaka hiyo mbele ya waandishi wa habari, Mkurugenzi mtendaji CPA Gilbert Kayange amesema zaidi shilingi milioni 800 ni deni lililotokana na wananchi kutokulipa ankara za maji.
Aidha CPA Kayange amesema mpaka sasa mkoa wa Mbeya ndio mkoa wenye vyanzo vingi vya maji ambapo kwa sasa mamlaka hiyo inavyanzo 29 ikiwa ni pamoja na mradi wa kimkakati wa mto kiwira ambao umefikia asilimia 40 ya ujenzi wake.
Hata Hivyo Katika Muendelezo wa Kuadhimisha Wiki Ya Maji Duninia, Mamlaka Ya Maji Safi Na Usafi Wa Mazingira Jijini Mbeya Imejianda Kutoa Elimu Kwa Wananchi Pamoja Na Kuzindua Miradi Mbalimbali Ya Maji inayotekelezwa jijini humo.
Kwa upande wake mhandisi Barnabas Konga mkurugenzi wa Ufundi amesema vyanzo vyote vya maji vinavyosimamiwa na mamlaka hiyo vinalindwa kwa kushirikiana na jamii na taasisi mbalimbali ikiwemo za umma na binafsi.
Maadhimisho ya wiki ya maji kwa Mwaka Huu Yanaongozwa Na Kaulimbiu Isemayo Kutunza Uoto Wa Asili Kwa Uhakika Wa Maji.