

18 March 2025, 19:43
Kutokana na changamoto ya wakulima wa kahawa wilayani Rungwe kuto kulipwa malipo yao ya Mwaka 2024, ameagiza kampuni iliyo nunua zao Hilo kulipa madai hayo ndani ya siku 14.
Na Ezra Mwilwa
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Steven Wasira ameiagiza Kampuni ya GDM kuhakikisha inalipa madeni ya wakulima wa kahawa wa Wilaya ya Rungwe ndani ya siku 14, baada ya malalamiko ya wakulima hao kuwasilishwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Machi 18, 2025 katika Stendi ya Mji Mdogo wa Tukuyu.
Wakulima hao wanadai malipo ya zaidi ya Shilingi milioni 600 kutoka kwa kampuni hiyo, wakisema ucheleweshaji wa malipo umewaathiri kwa kiasi kikubwa, huku wengi wakikosa fedha za kugharamia mahitaji yao na kuendeleza uzalishaji wa chai.
Akizungumza katika mkutano huo, Wasira amesisitiza kuwa serikali haitavumilia ucheleweshwaji wa malipo ya wakulima, akitoa onyo kali kwa kampuni hiyo kuhakikisha inatekeleza agizo hilo ndani ya muda uliowekwa.
Baadhi ya wakulima waliopata fursa ya kuzungumza walisema kuwa ucheleweshwaji wa malipo umewaathiri vibaya, huku wengine wakishindwa kulipia ada za watoto wao shuleni na kukidhi mahitaji yao ya kila siku.