Baraka FM

Baba adaiwa kutoweka na mtoto wake wa miezi Saba

23 February 2025, 07:50

Baba na mtoto(picha na Ezekiel Kamanga)

Katika Hali isiyo ya kawaida Baba anadaiwa kutoroka na mtoto wa miezi Saba, kwa madai ya MKE ametoa mwimba kwa njia za kishirikina.

Na Ezekiel Kamanga

Mariam Omary Said(21) mkazi wa Mabatini Jijini Mbeya anamtafuta mwanawe Muzdalifa Adamu Hinju jinsi ya kike mwenye umri wa miezi saba aliyetoweka na Baba Mzazi Adamu Hinju (27) tangu Februari 18,2025 jioni alipoaga kwenda kuchukua maziwa ya mtoto.

Mariam amesema mume wake amekuwa na kawaida ya kila siku jioni kwenda kufuata maziwa ya mtoto lakini siku hiyo hadi saa mbili usiku hakurejea nyumbani na alipomtafuta kwa simu haikuweza kupatikana hadi sasa.

Mariam Omary Said ambaye ni mama wa mtoto(picha na Ezekiel Kamanga)

Mariam Omary Said ametoa taarifa Kituo cha Polisi Kati Februari 20,2025 na kufunguliwa taarifa ya uchaguzi namba MB/RB/670/2025.

Numba ya mashitaka kutoka kituo cha jeshi la Polisi(picha na Ezekiel Kamanga)

Awali Mariam Omary Said amedai mumewe kumtuhumu kuwa alikuwa na mimba ambayo aliitoa kwa njia za kishirikina jambo ambalo amedai si kweli.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa msaada wa kisheria TALECACE Said Mohammed Madudu amekiri kupokea changamoto hiyo ofisini kwake na kumuomba Adam John Hinju kumrejesha mtoto kwa mama yake kwani bado ananyonya pia ni kinyume cha sheria na haki za binadamu.

Mkurugenzi wa msaada wa kisheria TALECACE Said Mohammed Madudu(picha na Ezekiel Kamanga)

Aidha amesema ni vema wanandoa hao kuzimaliza changamoto zao bila kuleta athari kwa mtoto.Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya zinaendelea Ili kujua hatua zilizofikiwa mpaka sasa ingawa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Anthony Mkwawa amekiri kulipokea suala hilo na kwamba linashughulikiwa.