Baraka FM

DSW yatoa mafunzo kwa Vijana,walimu na watalaamu wa afya chunya

6 December 2024, 18:47

Baadhi ya washiriki wa mafunzo(picha na Lukia Chasanika)

katika kuhakikisha sauti za vijana zinasikika ili kutokomeza ukatili wa kijinsia na kuwapatia huduma rafiki kwa afya ya vijana viongozi wa shirika la DSW Tanzania wamewakutanisha vijana,walimu na wataalamu wa afya Chunya mkoani Mbeya.

Na Lukia Chasanika

Vijana,walimu na wahudumu wa afya wametakiwa kuzingatia mafunzo yanayotolewa na shirika la DSW Tanzania kupitia mradi wa REST ili kuyatumia kuelimisha jamii inayowazunguka.

Hayo yamesemwa na afisa elimu vifaa na takwimu sekondari wilaya ya Chunya Costancia Komba akimwakilisha mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya chunya wakati akifungua mafunzo kwa walimu na vijana yaliyaandaliwa na shirika la DSW Tanzania kupitia mradi wa REST.

Sauti ya afisa elimu vifaa na takwimu sekondari wilaya ya Chunya Costancia Komba

Aidha mkurugenzi wa shirika la DSW Tanzania Peter Owaga amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapatia mafunzo washiriki kuimarisha mifumo iliyopo na kuhakikisha sauti za vijana zinasikika ili kutokomeza ukatili wa kijinsia na kuwapatia huduma rafiki kwa afya ya vijana.

Sauti ya Mkurugenzi wa shirika la DSW Tanzania Peter Owaga

Kwa upande wake afisa maendeleo ya vijana Joseph Sunge amelishukru shirika hilo kwa kupeleka mradi wa REST katika wilaya ya Chunya hususani tarafa ya Kipembawe ambako vijana wengi wapo katika mashamba ya tumbaku.

Washiriki wa mafunzo baada ya kuhitimisha mafunzo(picha na Lukia Chasanika)
Sauti ya afisa maendeleo ya vijana Joseph Sunge

Mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo kitaifa katika huduma rafiki kwa vijana Mariam Mhanjim amesema wanatoa mafunzo kwa watoa huduma namna ya kutoa huduma rafiki kwa kijana kulingana na mahitaji yao.

Sauti ya Mmoja wa wawezeshaji Mariam Mhanjim

Baadhi ya vijana walioshiriki katika mfunzo hayo wameahidi kuyafanyia kazi katika huduma mbalimbali za kijamii katika kata zao walizotoka za wilaya ya chunya.

Washiriki kutoka Idara ya Afya(picha na Lukia Chasanika)
Sauti za Baadhi ya vijana walioshiriki katika mfunzo hayo