Wazazi watakiwa kutowaozesha wanafunzi badala yake wawaendeleze kielimu
6 December 2024, 19:11
Kutokana na baadhi ya watoto kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao katika ngazi ya Elimu ya msingi na sekondari wazazi waazwa kuto kuwaozesha bari wawapatie nafasi ya kwenda kusomea fani mbalimbli katika vyuo vya kati na vyuo vikuu.
Na Hobokela Lwinga
Wazazi na walezi hasa wenye watoto wahitimu wa elimu ya msingi wametakiwa kuwaendeleza watoto wao kwa kuwapeleka kusoma elimu ya vyuo badala ya kubaki nyumbani na kuharibika KWA mfumo wa maisha yao ya badae.
Wito huo umetolewa na makamu mwenyekiti wa Kanisa La Moravian Tanzania Jimbo La Kusini Magharibi mch.Asulumenye Mwahalende katika mahafali ya nane ya chuo cha Ufundi Ilindi kinachomilikiwa na jimbo hilo kilichopo halmashauri ya wilaya ya mbeya.
Mch.Mwahalende amesema vyuo vimekuwa na mchango mkubwa kwa taifa kwani vimekuwa vikipunguza ukosefu wa ajira kwa vijana wengi kutokana na kwamba wamekuwa wakijiajiri.
Mch.Mwahalende ameongeza kuwa kama kanisa watahakikisha wanatengeneza mazingira mazuri kwa vijana wanaosoma katika vyuo vya kanisa ikiwa ni pamoja na kuongeza fani mbalimbali pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya kujifunzia.
Akihuhubiri katika mahafali hiyo mchungaji wa wanafunzi katika chuo hicho Musa Mwamwezi amesema wanafunzi hao wanatakiwa kutambua kuwa katika mafanikio ya elimu yao wamewezeshwa na Mungu mwenyewe.
Hata hivyo risala ya mkuu wa chuo imeeleza uwepo wa mafanikio kadhaa yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa chuo hicho ikiwa ni pamoja na ongezeko la wanafunzi.
Kwa upande wa risala ya wanafunzi iliyosomwa na na Sarah Boniface Mwangwaleimetoa shukrani kwa kanisa na ufadhili wanaoupata wa kupatiwa elimu.
Hiki ni chuo cha tatu cha ufundi cha Kanisa La Moravian Tanzania Jimbo La Kusini Magharibi kikitanguliwa na chuo mama cha Ufundi Moravian Kadege MVTC na chuo cha ufundi chunya ambavyo vyote vinapatikana mkoani mbeya.