Baraka FM

CBE yapongezwa na serikali kwakutoa Elimu bora ya uchumi

3 December 2024, 06:48

Baadhi ya wakufunzi wa chuo cha elimu ya biashara nchini CBE(picha na Ezra Mwilwa)

Katika kuhakikisha vyuo vinaendelea kutoa Elimu bora Naibu Waziri wa viwanda na biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe amepongeza juhudi zinazo fanywa na wakufunzi wa chuo cha elimu ya biashara nchini CBE.

Na Kelvin Lameck

Serikali imesema inatambua na kuthamini mchango wa chuo cha elimu ya biashara nchini CBE katika kuzalisha wataalam mahiri ambao wanachangia kujenga uchumi wa viwanda.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa viwanda na biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe wakati akiwa katika mahafali ya 59 na ya 11 kwa kampasi ya Mbeya yaliyofanyika chuoni hapo.

Naibu Waziri wa viwanda na biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe(picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya Naibu Waziri wa viwanda na biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe

Aidha Mkuu wa vyuo vya CBE nchini Profesa Edda Tandi Lwoga amesema Jumla ya wahitimu 5306 wamehudhurishwa katika kampasi zote za chuo cha CBE ambapo kwa kampasi ya Mbeya wanafunzi 314 wamehudhurishwa.

Sauti ya Mkuu wa vyuo vya CBE nchini Profesa Dr. Edda Tandi Lwoga

Naye Makamu Mwenyekiti wa bodi ya uongozi wa chuo Dk. Kennedy Hosea amesema kwa mara ya kwanza chuo cha CBE kinatarajia kuanza kutoa double degree kwa wakati mmoja.

Baadhi ya wahitimu wa chuo cha Elimu na Biashara kampasi ya Mbeya(picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa bodi ya uongozi wa chuo Dk. Kennedy Hosea

Kwa upande wake Mhadhiri wa chuo cha elimu ya biashara CBE Mbeya Dr. Beni Mwenda amewataka wahitimu wote kutumia maarifa waliyoyapata chuoni hapo sambamba na kutimiza malengo yao.

Sauti ya Mhadhiri wa chuo cha elimu ya biashara CBE Mbeya Dr. Beni Mwenda