Jamii imetakiwa kusaidia watu wenye mahitaji maalumu
17 October 2024, 15:43
Kumekuwa na familia nyingi zinazoishi katika hali duni za maisha kwa kutambua hilo kila mtu anawajibu wa kusaidia jamii hizo ili kuondokana na changamoto zinazozikabili.
Na Flora Godwin
Kikundi Cha Iyela Mamas wameto msaada kwa wahitaji zaidi ya 50 wakijumuishwa wazee, wajane na watoto yatima.
Akizingumza na kituo hiki mwenyekiti wa kikundi hicho Scora Asey amesema Group hilo linajumla ya wanafamilia 106 na lengo lao ni kuhudumia watu wenye uhitaji maalumu lakini pia wamekuwa na malengo ya kuwaandaa watoto wakike kuwa viongozi bora wa baadae.
Lakini pia ameviomba baadhi ya vikundi vinavyo jihusisha na mambo ya kijamii kuzingatia pia wahitaji walioko majumbani sio kuwahudumia wale tu wanaopatikana katika maeneo maalumu.
Kwa upande wake Zamira Muihojo ambaye ni katibu wa Iyela Mamas amewashukuru wanachama wa kikundi hicho kwa namna walivyojitolea kwa wahitaji hao.
Nao wanachama wa Iyela Mamas wanawashukuru viongozi wao kuwa na maono bora na yenye tija kwenye kundi lakini pia kwa jamiii inayo wazunguka.
Wakizungumza baada ya kupokea msaada huo baadhi ya wahitaji hao wamewashukuru wanafamilia hao kwa upendo wa dhati walio uonyesha kwa upendo wao.
Elisha Pita ni afisa mtendaji wa mtaa wa Iyela 1 amesema kikundi hicho kimekuwa msaada mkubwa kwenye jamii nakutaka baadhi ya vikundi kuiga mfano huo.