Baraka FM

Mradi wa REGROW watoa fursa kwa wananchi kutoa malalamiko yao

8 October 2024, 12:00

Ewe mwananchi mradi wa REGROW Unaofadhiliwa na bank ya dunia unakupa fursa ya kutoa malalamiko yako endapo unaipata changamoto katika uhifadhi, ukatili wa kijinsia, sambamba  na migogoro ya ardhi.

Njia za kutoa malalamiko

1. Fika ofisi za Kijiji chako, utapokelewa na kisha malalamiko yako yatashughulikiwa.

2. Piga simu bure kupitia hifadhi ya taifa ya Ruaha 0800 110 801 au wizara ya Mali asili na utafiti 0800 110 804.

3. Toa malalamiko yako kupitia www.emrejesho.gov.go.tz

4.Lakini pia unaweza kutuma malalamiko yako kupitia mfumo wa Serikali wa e- Mrejesho mtandaoni kwa kutembelea www.emrejesho.gov.go.tz, au piga *152*00# kisha chagua 9, alafu chagua 2 ili kuufikia mfumo wa e-Mrejesho. Hapo utaweza kutoa malalamiko yako.

Malalamiko yatasikilizwa kwa umakini, na utapata mrejesho mara moja. Hifadhi ya Taifa Ruaha na Mradi wa REGROW wanahakikisha usalama na ustawi wa jamii yako.