Madereva, makondakta Mbeya waomba kazi yao iheshimiwe
3 September 2024, 18:52
Sekta ya usafirishaji ni sekta inayotegemewa kwa kiwango kikubwa kutokana na uwepo wa sekta hiyo ajira nyingi zimetengenezwa licha ya uwepo wa changamoto wanazokutana nazo watendaji katika sekta hiyo.
Na Hobokela Lwinga
Baadhi ya maafisa usafirishaji na madereva wa daladala Jijini Mbeya wameomba abiria na watumiaji wa vyombo vya usafiri wa umma kubadili mtazamo uliopo juu yao na kuheshimu kazi wanaoyoifanya kwani ni kazi kama zilivyo kazi zingine.
Katika mahojiano na kituo watoa huduma hao, wamelalamikia jinsi jamii inavyowahusisha na watu wengine wenye tabia zisizofaa ikiwemo ulevi wakisema kuwa wengi wao wanajituma na wanatumia kazi hiyo kuhudumia familia zao.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini humo wameeleza kuwepo kwa baadhi na watoa huduma kuwa na tabia zisizofaa huku wengine wakitoa lugha zisizofaa ikiwemo matusi jambo ambalo halileti afya.
Naye kiongozi anayesimamia wakati wa kuandikisha foleni ya gari zinazofanya safari zake Mbeya, Tukuyu, Kyela ( Mbetuke) Victor Mwakapyela amesema kuwa wameamua kuweka utaratibu wa gari hizo ili kudhibiti ajali zilizokuwa zikitokea mara kwa mara.