DED mpya Mbarali awataka watumishi wa halmashauri kuzingatia weledi
21 August 2024, 13:46
Unapopewa nafasi ya kusimamia jambo lolote unapaswa usimamie ili matokeo chanya yaonekane, na usipotekeleza unapoteza imani kwa mtu aliyekuamini na kukupa nafasi hiyo ya usimamizi.
Na Hobokela Lwinga
Mkurugenzi Mpya wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya Stephen Katemba amewataka watendaji wa halmashauri hiyo kutimiza wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao katika nafasi wanazozitumikia.
Ameyasema hayo katika kikao chake cha Kwanza baada yakupokelewa na watumishi hao katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali.
Mhe. Katemba Amesema kila mtumishi anapaswa kufanya kazi huku akijua kufanya hivyo ni kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Aidha amesema kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi watumishi hao wanapaswa kufanya kazi ya usimamizi wa miradi ili watakaopewa nafasi ya kugombea nafasi mbalimbali wawe na nguvu ya kusema kuwaambia wananchi namna Rais alivyotekeleza miradi katika maeneo yao.
Katika hatua nyingine amewashukru viongozi waliopita kabla yake katika halmashauri hiyo akiwemo mkuu wa wilaya na mkurugenzi.
Ikumbukwe kuwa mhe.Stephen Katemba kabla ya kuhamishiwa katika katika halmashauri ya wilaya ya Mbarali aliwahi kutumika katika halmashauri ya Mbeya na sumbawanga mkoani Rukwa kama mkurugenzi.