Baraka FM

Wananchi Igodima waomba kujengewa ofisi ya mtaa

16 August 2024, 22:22

Baadhi ya wananchi mtaa wa Igodima Mbeya (picha na Hobokela Lwinga)

Katika kurahisisha upatikanaji wa huduma bora na karibu na wananchi hurahisishwa na ofisi zilizo karibu,katika mtaa wa Igodima jijini Mbeya kwao hali hiyo imekuwa tofauti na wananchi wa mitaa mingine.

Na Hobokela Lwinga

Baadhi ya wananchi mtaa wa Igodima Kata Ya Iganzo Jijini Mbeya,wameiomba Serikali Kuwajengea Ofisi Ya Mtaa Katika eneo hilo kwaaajili ya kurahisisha upatikanaji Wa huduma za ziserikali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Na Baraka fm wananchi hao wamesema kukosekana kwa ofisi ya mtaa katika Eneo hilo imekuwa ni changamoto kwao hivyo kushindwa kupata huduma za kiserikali kwa wakati.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Ayoub Mwanzele amekiri wazi kutokuwepo kwa ofisi na kwamba serikali ya ntaa ipo katika ujenzi wa ofisi Na inatarajiwa kukamilika siku za hivi karibuni.

Naye Diwani Wa kata hiyo ya Iganzo Daniel Mwanjoka amesema ofisi ya mtaa wa Igodima ipo Na inaendelea kujengwa ndani ya mtaa huo ambapo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mapema na tayari kwa kuanza kutumika.