Baraka FM

Watoto wenye ulemavu, yatima wapokea misaada kutoka kwa wadau wa Baraka FM

3 July 2024, 14:32

Baadhi ya watoto waliofika kupokea msaada wa wadau wa Baraka fm(picha na Hobokela Lwinga)

Wahenga wanasema kutoa ni moyo si utajiri, ukisoma vitabu vitakatifu navyo vinasisitiza kutoa ni ibada hivyo kila mtu anapaswa kuona umuhimu wa kumsaidia mtu yeyote mwenye uhitaji.

Na Hobokela Lwinga

Mahitaji mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja yametolewa na wadau Kwa kushirikiana na kituo Cha redio Baraka kwa watoto wenye ulemavu na yatima katika kata ya Ubaruku halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Akizungumza mbele ya mamia ya wazazi walifika kushuhudia tendo hilo,mwenyekiti Wa wadau bw.Christopher Sengo Amesema wametembelea shule ya msingi yenye watoto walemavu ya Ubaruku na kituo cha watoto yatima Cha hope of Tanzania.

Amesema katika vituo hivyo wametoa mahitaji ya shule ikiwemo daftari, chakula, nguo pamoja na fedha taslimu zaidi ya laki moja.

mwenyekiti Wa wadau bw.Christopher Sengo(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mwenyekiti Wa wadau bw.Christopher Sengo

Charles Amlike ni meneja wa redio baraka Amesema zawadi hizo zimetokana na wadau ambao wameguswa, hivyo amewataka wapokeaji kuendelea kuwaombea kwani  nao wanahitaji kufunguliwa kwenye maeneo yao.

Charles Amlike ni meneja wa redio baraka(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Charles Amlike ni meneja wa redio baraka

Kwa upande wao Mkuu wa shule ya msingi Ubaruku Damiana Sanga na mwenyekiti Wa kituo cha hope of Tanzania  Clemence Julias Mwakoga msaada hiyo itasaidia kutoa motisha na changamoto zinazowakabili watoto hao ikiwemo mavazi na chakula.

Mkuu wa shule ya msingi Ubaruku Damiana Sanga(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti za Mkuu wa shule ya msingi Ubaruku Damiana Sanga na mwenyekiti Wa kituo cha hope of Tanzania  Clemence Julias Mwakoga

Mmoja wa wazazi ameshukru kwa msaada uliotolewa huku akiomba wadau hao wasiache kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Sauti ya mmoja ya wazazi