Baraka FM

Kwaya kuu kanisa la Moravian jimbo la kusini magharibi wafanya ziara Uswiss

20 June 2024, 18:48

Baadhi ya wanakwaya walio Shiriki ibada hiyo Uswiss

Baadhi ya Wanakwaya ya Wawakilishi Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi wakiwa nchi ya Uswiss

Na Ezekiel Kamanga

Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mchungaji Asulumenye Ever Mwahalende ameongoza Kwaya ya Jimbo katika ziara Ushirika wa Diepoldsau Uswiss.

Ziara hiyo imeanza Juni 17,2024 ikiwa na Jumla ya waimbaji kumi na nane ambapo ina jumuisha waimbaji kutoka shirika mbalimbali za Jimbo la Kusini Magharibi.

Baadhi ya wanakwaya wawakilishi wakiwa Uswiss

Mratibu wa Kwaya Angelica Sulusi amesema lengo la ziara hiyo ni kubadilishana vipawa vya uimbaji na kazi za mikono baina ya shirika za Uswiss na Jimbo la Kusini Magharibi.

Waimbaji wa kwaya kuu ya Jimbo la kusini magharibi

Ziara hii ni muendelezo wa ushirikiano baina ya Kanisa la Moravian Uswiss na Jimbo la Kusini Magharibi ambazo nimekuwa zikifanyika mara kwa mara ili kuujenga mwili wa Kristo.

Sulusi amesema Kwaya ya Jimbo itatembelea shirika mbalimbali na maeneo ya historia ya Kanisa la Moravian Duniani.