Serikali kupunguza kero kukatika umeme kwa kuanzisha njia mbadala
12 June 2024, 14:43
Shirika la umeme TANESCO limeboresha huduma za nishati hiyo na kupunguza kukatikatika kwa umeme kwenye maeneo mengi nchini.
Na Hobokela Lwinga
Serikali kupitia shirika la umeme Tanzania TANESCO linatekeleza uanzishwaji wa vyanzo mbalimbali vya uzalishaji umeme ili kuondokana na kero ya kukatika mara kwa mara.
Akizungumza na kituo hiki Afisa uhusiano na huduma kwa wateja Christina Shoki amesema vipo vyanzo mbalimbali vimebuniwa nje na bwawa la mwalimu nyerere ambavyo ni uzalisha wa umeme kwa njia ya upepo na solar kwa baadhi ya mikoa.
Aidha amewaomba wananchi kutoa taarifa wanapoona uharibifu wa miundo mbinu ya umeme ili shirika la Tanesco liweze kutatua haraka changamoto hizo.
Kwa upande wake Afisa usalama wa shirika hilo mkoa wa Mbeya Aloyce Mndolwa amekiri kuwepo kwa vishoka hivyo jitihada kubwa zimefanyika za kukabiliana na watu hao na wamefanikiwa kuwapunguza.