Baraka FM

Wananchi washiriki mdahalo wa wazi wa katiba,waomba mchakato uharakishwe

12 June 2024, 14:04

Katiba Ni Muongozo Ambao Unawekwa Kwa Ajili Ya Kuongoza Mambo Mbalimbali Iwe Katika Nchi,Vikundi Hata Taasisi Mbalimbali.

Na Deus Mellah

Chama cha Wanasheria wa Tanganyika TLS kinaendelea kuendesha mijadala ya wazi yenye kujenga, kusikiliza na kupokea maoni ya Wananchi kuhusu namna bora itakayosaidia kupata katiba mpya.

Akizungumzia suala hilo Rais mstaafu wa Chama cha wanasheria wa Tanganyika TLS Wakili Francis Stolla amesema kwa mujibu wa katiba ya sasa baadhi ya viongozi wana kinga ya kutoshtakiwa jambo ambalo sio sawa.

Rais mstaafu wa Chama cha wanasheria wa Tanganyika TLS Wakili Francis Stolla(picha na Josea Sinkala)
Sauti ya Rais mstaafu wa Chama cha wanasheria wa Tanganyika TLS Wakili Francis Stolla

Aidha mmoja wa watoa mada Mjumbe wa bodi ya jukwaa la katiba nchini Tanzania Deus Kibamba ameainisha madhaifu mbalimbali ya katiba ya sasa.

Mjumbe wa bodi ya jukwaa la katiba nchini Tanzania Deus Kibamba(picha na Josea Sinkala)
Sauti ya Mjumbe wa bodi ya jukwaa la katiba nchini Tanzania Deus Kibamba

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi amesema katiba mpya ni hitaji la wananchi la muda mrefu pamoja na tume huru ya uchaguzi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi(picha na Josea Sinkala)
Sauti ya mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi

Kwa upande wao baadhi ya wananchi kutoka makundi mbalimbali katika jamii Mkoani Mbeya wameiomba serikali kuharakisha mchakato wa mabadiliko ya katiba ili iendane na wakati uliopo.