Baraka FM

Waandishi wa habari Mbeya kuwezeshwa kuandika habari za uchaguzi

15 May 2024, 19:06

Baadhi ya waandishi wa habari na wanachama wa Mbeya press club katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Mbeya mhe.Beno Malisa(wa pili kushoto walio kaa)-picha na Hobokela Lwinga

Tanzania inatarajia kuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 na moja ya tasnia inayotazamwa kutoa elimu ni vyombo vya habari kutokana na kuwa karibu na jamii.

Na Hobokela Lwinga

Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya imesema iko tayari kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari ili kuandika habari zenye mlengo wa kutoa elimu juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 wa madiwani,wabunge na Rais.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe.Beno Malisa wakati akimuwakilisha Mkuu mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera kwenye sherehe za Uhuru wa vyombo vya habari mkoa Mbeya zilizofanyika katika ukumbi wa coffee gadern jijini Mbeya.

Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Mbeya wakifuatilia kwa ukaribu ratiba inayoendelea katika maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari Mbeya (picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe.Beno Malisa

Aidha mhe.Malisa amewataka waandishi hao wa habari mkoani hapa kutumia fursa zinazojitokeza kwenye maeneo yao.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe.Beno Malisa

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amewataka waandishi kuwa weledi katika kutekeleza majukumu yao.

Mkuu wa wilaya Mbeya mhe.Beno Malisa (aliyesimama)(kulia) ni kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe.Beno Malisa

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga Amesema wanahabari wamekuwa watu muhimu kwenye jamii kutokana na mchango mkubwa wa kuhabarisha umma huku akiwataka kuendelea kufichua vitendo vya uharifu vinavyofanywa na watu wasio wema.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga

Awali akiwasilisha risala ya waandishi wa habari kwa mgeni rasmi,Katibu mkuu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya Elizabeth Nyivambe amesema uwepo wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya umesababisha taaluma ya habari kukua sambamba na kuongezeka kwa ufikishwaji wa taarifa kwa jamii.

Katibu mkuu wa chama cha waandishi wa habari wa Mbeya Elizabeth Nyivambe (picha na Hobokela Lwinga).
Sauti ya Katibu mkuu wa chama cha waandishi wa habari wa Mbeya Elizabeth Nyivambe

Katika maadhimisho hayo yamekwenda na kauli mbiu inayosema Uandishi wa habari na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.