Ng’ombe azaa ndama mwenye miguu mitano na jinsia mbili Mbeya
11 May 2024, 12:47
Katika hali ya kustahajabisha ng’ombe anamiguu minne lakini maajabu yametokea ndama kazaliwa akiwa na miguu mitano na jinsi zote mbili (jike na dume)
Na Mwandishi wetu,Mbeya
Ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni, ndivyo tunaweza kusema kufuatia tukio la kuzaliwa kwa ng’ombe(ndama)mwenye miguu mitano na jinsia mbili(jike&dume) katika eneo la kijiji cha Kapugi kata ya Malindo wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
Akizungumzia na kituo Bwana Lusubilo Abonike ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kapugi na mmiliki wa ng’ombe huyo ambaye amezaa ndama mwenye miguu mitano na jinsia mbili (dume na jike) amesema alistaajabishwa sana baada kushuhudia ng’ombe wake amezaa ndama wa maajabu.
Nao baadhi ya mashuhuda watukio hilo wameiomba serikali kuwasaidia kutoa taharuki kwani limewatisha huku wakihusisha na imani za kishirikina.
Hata hivyo wenyekiti wa kijiji cha Kapugi Ikumboka Kasege amesema tukio hilo kwenye eneo lake ni la kushangaza kwani halijawahi tokea.
Kwa upande wake afisa ugani wa kijiji cha Kapugi Bwana Batweli Mbilinyi amesema kuwa kuzaliwa kwa ndama wa aina hiyo ni suala la kawaida na linasababishwa na sababu la kibaiolojia.