Viongozi wa dini waja na mkakati kabambe kilimo cha ufuta
25 April 2024, 21:39
Kwa kutambua umuhimu wa kilimo nchini, taasisi za dini zimejikita katika uzalishaji wa mazoa biashara katika kilimo cha ufuta.
Na Ezra Mwilwa
Umoja wa Makanisa Tanzania umejipanga kuanzisha mradi wa kilimo cha ufuta ili kuinua uchumi wa nchi. Kauli hiyo imetolewa na Askofu Prof. Silivesta Gamanywa wakati akizungumza na wanahabari jijini Mbeya baada ya kukamilika kwa mkutano uliowakutanisha viongozi wa makanisa mbalimbali utakaotekelezwa katika wilaya ya Kilwa kwa ufadhili kutoka serikali ya Israel.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Maprofesa na Madaktari wa Teolojia Tanzania Prof. Rejoice Ndalima amesema katika kipindi hiki cha ukuaji wa teknojia ya kilimo ni vema watu kujiwekeza katika kilimo cha kisasa cha ufuta.
Askofu Gamanywa ameongeza kuwa kanisa linaanzisha mradi huo kwa kuzingatia soko kubwa la ufuta duniani.