Wanyakyusa kufanya tamasha la utamaduni Makumbusho Dar es Salaam
22 April 2024, 09:25
Kutokana na Makumbusho ya Taifa kufanya matamasha mbalimbali ya kitamaduni kote nchini mwaka huu, kabila la wanyakyusa linalopatikana katika halmashauri za Rungwe na Kyela mkoani Mbeya linatarajia kufanya tamasha lao katika jiji la Dar es salaam.
Na Ezra Mwilwa
Kuelekea tamasha kubwa la kabila la wanyakyusa kitaifa litalo fanyika Makumbusho Dar es salaam tarehe 26-28/7/2024 wananchi wametakiwa kudumisha na kuenzi asili ya makabila yao huku wakihimizwa kujitokeza kushiriki tamasha hilo.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera.
Mhe. Malisa amesema wanyakusa wote wajitokeze kushiriki tamasha hilo pamoja na makabila mengine ili kuendelea kudumisha mila na Desturi za makabila yao.
Mhifadhi na mtafiti kutoka Makumbusho ya Taifa Flora Vicent amesema lengo la kufanya matamasha haya nikuzipatia jamii nafasi ya kuweza kuonyesha mila na desturi zao kwa watu wa jamii tofauti tofauti.
Nae mwenyekiti wa kamati ya ushauri na ufadhili Martha Mwaijande amesema wao kama wanyakusa wanaamini katika kipindi hiki cha ukuaji wa teknolojia na sayansi ni vema wakakumbushana tamaduni zao.