Mhandisi Merryprisca Mahundi atoa msaada kwa waathirika wa maporomoko Mbeya
18 April 2024, 18:17
Kutokana na Mvua zinazonyesha kusababisha maporomoko katika kata ya Itezi jiji Mbeya na kusababisha wakazi kukosa maeneo ya kuishi huku wengine wakipoteza mali pamoja na mifugo wadau mbalimbali wameendelea kutoa misaada ya kujikimu kwa wahanga hao.
Na Ezra Mwilwa
Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation(MWEF)inayoongozwa Mhandisi Maryprisca Mahundi Naibu Waziri wa Habari Teknolojia ya Mawasiliano na Habari,Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya imejitokeza kutoa msaada kwa waathirika wa maporomoko ya mlima Kawetere Kata ya Itezi Jijini Mbeya.
Baraka Mlonga ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation(MWEF)amesema Mkurugenzi wake Mhandisi Maryprisca Mahundi alitamani kuwepo lakini yupo nje ya nchi hivyo wapokee msaada huo na uwe faraja kwa waathirika.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Itezi Sambwee Shitambala mbali ya kushukuru kupokea msaada huo ameomba wasisisite kurudi tena kwani bado msaada unahitajika zaidi.
Neno la shukurani kwa niaba ya waathirika ilmetolewa na Upendo Mwakasendo ambaye amewashuru wote walioguswa kuwasaidia katika kipindi hiki kigumu wanachopitia kwani wengi wao wamepoteza kila kitu vikiwemo vyakula,mavazi na fedha.
Bado msaada wa kibinadamu unahitajika sana kwa wananchi hao vikiwemo vyakula,nguo na malazi kutokana na wananchi hao baadhi kushindwa kuokoa vitu vyote vilivyokuwemo ndani.